SIMBA YAPIGWA TAFU TENA NA SPORTPESA, BADALA YA MIL 888 SASA NI MIL 950 KWA MWAKA

Siku chache baada ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kuingia mkataba wa miaka mitano, taarifa zinaeleza sasa mkataba huo utaboreshwa zaidi.

Taarifa za uhakika tokea ndani ya Simba zimeeleza mkataba huo utaboresha kutoka kitita cha Sh milioni 888 kwa mwaka hadi Sh milioni 950.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, awali mkataba walioingia Simba ulikuwa ni Sh bilioni 4.9 kwa miaka mitano lakini sasa mkataba huo utakuwa ni Sh bilioni 5.173.

Taarifa zimeeleza kwamba Yanga na SportPesa wanaingia mkataba huo rasmi leo na utakuwa ni sawa kabisa na huo wa Simba baada ya kuboreshwa.

Yanga pia watalipwa Sh bilioni 5.173 kwa mwaka na kufanya timu hizo ziwe zinalipwa sawa kila kitu.


EmoticonEmoticon