AHUKUMIWA JELA MIEZI 12 KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

MKAZI  wa kijiji cha Lyapinda tarafa ya Wampembe wilayani Nkasi mkoani Rukwa Derick simfukwe (25) amehukumiwa kwenda  jela miezi 12 au kulipa faini ya Tsh LAKI 5 na mahakamama ya wilaya Nkasi kwa kosa la kukutwa na Nyara za serikali.

Mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo mbele ya Mahakama  huku akiiomba mahakama hiyo isimpatie adhabu yoyote kwa maana hakujua kuwa mnyama huyo aina ya Insha ni nyara ya serikali.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhani Rugemalila ,amesema mtuhumiwa amekutwa  na  hatia  baada  ya  kutenda  kosa  hilo .

Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe ni fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutaka kutenda kosa kama hilo.


EmoticonEmoticon