REAL MADRID KUJITENGENEZEA NJIA YA UBINGWA WA LA LIGA LEO DHIDI YA CELTA VIGO

LEO, Real Madrid wako Ugenini huko Estadio Balaidos kucheza Mechi yao ya Kiporo na Celta Vigo na ushindi kwao utawaweka Pointi 3 mbele ya Barca huku Mechi zikibaki 1 kwa kila Timu.
La Liga itafikia tamati Jumapili Mei 21 na hadi sasa Barca na Real ziko juu kileleni zikifungana kwa Pointi lakini Barca wanaongoza kwa Rekodi yao Bora ya uso kwa uso na Real.
 
Hata hivyo, Real wana Mechi 1 mkononi na ndio hiyo wanayocheza leo na wakishinda leo basi Jumapili kwenye Mechi yao ya mwisho Ugenini na Malaga watahitaji Sare tu ili watwae Ubingwa wao wa kwanza wa La Liga tangu 2012. 
 
Hivi sasa Celta Vigo wapo Nafasi ya 13 kwenye La Liga na hawajashinda mechi tangu katikati ya Mwezi Aprili wakifungwa Mechi 6 kati ya 7 walizocheza tangu wakati huo ambapo pia walitupwa nje ya Nusu Fainali ya Europa League na Manchester United.
 
Licha ya takwimu hizo, Kocha wa Real, Zinedine Zidane, amesisitiza mechi hii ni kama fainali kwao huku akithibitisha kuwemo Kikosini mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo.
 
Nae Kocha wa Celta Vigo, Eduardo Berizzo, amesisitiza mechi hii ni nafasi safi kwao kufuta matokeo mabovu yao ya hivi karibuni. 
 
Katika mechi ya Kwanza ya La Liga msimu huu iliyochezwa mwezi Agosti huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Real iliichapa Celta Vigo 2-1 kwa bao za Alvaro Morata na Toni Kroos wakati lile la Celta lilifungwa na Fabian Orellana.
 
LA LIGA 
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumatano Mei 17
22:00 Celta Vigo v Real Madrid 
Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
21:45 Granada v Espanyol 
Jumamosi Mei 20
18:00 Deportivo v Las Palmas 
18:00 Sporting Gijon v Real Betis 
18:00 Leganes v Alaves 
Jumapili Mei 21
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club 
17:45 Celta Vigo v Real Sociedad 
17:45 Sevilla v Osasuna 
17:45 Valencia v Villarreal 
21:00 Barcelona v Eibar 
21:00 Malaga v Real Madrid


EmoticonEmoticon