WANANCHI NATOLIA WANALAZIMIKA KUNYWA MAJI YA MADIMBWI.


Safina Sarwatt,Arusha.

WANANCHI wa jamii ya wafugaji (wamasai) katika  vitongi  viwili vya
Natolia na Engusero kata ya Makuyuni wilayani Monduli mkoani  Arusha
wanalazimika kunywa maji ya madimbwi na mifereji  kwa zaidi ya miaka
33 jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Wakizungumza na gazeti hili mwisho mwa wiki hii katika kata ya
Makuyuni  wananchi hao walisema kuwa tangu kuzaliwa kwao hawajawahi
kuona wala kutumia maji ya bomba.

Meleji Mboika amesema kuwa wamekuwa wakitumia  maji ya  madimbwi na
mifereji kwa matumizi ya kunywa pamoja na matumizi mbalimbali ya
majumbani na mifugo.

Amesema kuwa tatizo hilo la maji limekuwa la muda mrefu lakini hakuna
majibu sahihi linalotolewa na serikali pamoja na viongozi huko
wananchi wakiendelea kuteseka.

Asiah Nainyoki  amesema kuwa wanashindwa kufanya shughuli za
uzalishaji  wa mali na badala yake wamekuwa  wakilazimika kutembea
kilometa 15 hadi 20 kutafuta maji safi na salama.

Awali akipokea msaada wa ng’ombe sita  waliotolewa na shirika lisilo
la kiserikali la Eagle Wings Enlightenment Center kutoka jimbo la
California nchini Marekani mwenyekiti wa kijiji cha Natolia kata
Makuyuni Wiliam Sanare,alisema kuwa tangu mwaka 1983 wananchi kijiji
cha Naitolia wamekuwa wakutumia maji madimbwi kwa kunywa.

Sanare amesema kuwa  tatizo hilo limekuwa kero kubwa kwa wananchi
jambo ambalo linawalizimu wananchi kutumia maji dimbwi pamoja na
ng’ombe.

Mbali na hayo pia alipongeza shirika hilo kwa toa msaada huo wa
ng’ombe mbapo alisema kuwa msaada utawasaidia wananchi kujikwamua
kiuchumi.

Amesema kuwa kijiji hicho mwaka 2009 ilikubwa na ukame uliosababisha
mifungo zaidi ya 2000 kufa ambapo wananchi wengi hawakufidiwa ng’ombe
zao.


EmoticonEmoticon