KM12 ZA BARABARA MOSHI KUWEKWA CHANGARAWE

Safina Sarwatt,Moshi,

SERIKALI  katika halmashauri ya Moshi ,mkoani Kilimanjaro imeanza
ujenzi wa barabara yenye  ukubwa wa  kilomita 12 kwa kiwango cha
changarawe.

Mradi huo wa Barabara zinazojengwa ni kuanzia Pofo-mandaka –hadi
kilema  ambazo zinaurefu wa kilomita 14 .

Hata hivyo  zabuni ya matengenezo  ya barabara hizo itaigharimu kiasi
cha shilingi 485,465,200 ambao  unakadiriwa kukamilika mwezi  mwishoni
mwa mwezi Novemba  mwaka huo.

Kwa mujibu wa  mkurugenziwa halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Butamo
Ndalahwa amesema lengo la mradi huo  nikuboresha  miundombinu  ili
kurahisisha  utoaji  wa huduma  zakijamii,kiuchumi na kiusalama na
kuondoa  kero.

Aidha amesema kwa mwaka fedha 2015/16  Halmashauri ya Moshi ilipokea
fedha  kutoka serikalini kiasi cha shilingi milioni 496.16 kwa ajili
ya matengenezo ya barabara ya pofo-mandaka hadi kilema.

Ndalahwa pia alimtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo
kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha juu kulingana na mkataba
mlioafikianana halmashauri.

Kwa upande wake mkandarasi anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo,kutoka
kampuni ya Termite Investment ltd, Injinia loomon olesingo amesema
kuwa changamoto kubwa wanayoipata ni kukosekana kwa maji ya uhakika
kutokana na watu wanaouishi maeneo hayo wamekuwa wakienda katika
chanzo cha maji nakuvunja kingo za sehemu zile zinayopitisha maji  .


EmoticonEmoticon