SERIKALI imeamua kulirejesha mikononi mwa halmashauri ya wilaya ya Hai
mkoani Kilimanjaro, shamba la Fofo estate lenye ukubwa wa ekari 105
baada ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa kugombea shamba hilo,
baina ya wananchi wa vijiji vinne vya urori, tella, mula na
Usalivilivyopo wilayani humo.
Uamuzi huo wa kulirejesha shamba hilo umetangazwa jana na Mkuu wa
Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa, wakati wa mkutano mkuu wa kijiji
uliofanyika katika kijiji cha Fofo wilayani humo.
Shamba la Fofo estate lililoko wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro,
limerejeshwa mikononi mwa halmashauri baada ya kuwepo kwa mgogoro wa
muda mrefu kati ya Wananchi wa eneo lililoko shamba hilo na mtu
anaedaiwa kuwa ni mmiliki wa shamba hilo Peter Karanti.
Amesema mbali na ukiukwaji huo, Karanti aliendelea na harakati za
kutafuta umiliki wa shamba hilo huku akijua wazi ya kuwa utaratibu huo
hauruhusu kufuatia ukiukwaji alioufanya.
Kuhusu fidia alizokuwa akidai, Karanti na wenzake walizokuwa wakiidai
serikali, Bw. Byakanwa alisema serikali haiwezi kuilipa kwa vile ardhi
ni mali ya serikali yenyewe.
Aidha amesema atamshauri Waziri mwenye dhamana ya ardhi
kuridhia uamuzi huo na kwamba uongozi wa wilaya ya Hai umezuia aina
yeyote ya shughuli zote kwenye shamba hilo.
Mkuu huyo wa wilaya aliulekeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya
Hai, kupima shamba hilo na kutenga maeneo kulingana na mahitaji ya
matumizi mbalimbali.
Uamuzi huo umekuja baada ya mgogoro wa shamba hilo lenye ukubwa wa
ekari 105 kudumu kwa zaidi ya miaka 40.
Awali shamba hilo lilikuwa likimilikiwa na Dkt Anthony Phoneas miaka
ya 1960 kabla ya kumilikishwa kwa wanachama wa chama cha ushirika wa
Narumu Manushi.
EmoticonEmoticon