TRA YAWATAKA WANANCHI KULIPA KODI BILA KUSHURUTISHWA



SAFINA SARWATT,MOSHI


MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imewataka wananchi kulipa kodi bila kushurutishwa ili kuharaikisha ukuaji wa uchumi wa taifa.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi (tra)Richard Kayombo amesema endapo kila mtanzania atawajibika kulipa kodi nchi itakuwa na uwezo wa kujiendesha bila kutegemea misaada ya wafadhili.

Amesema nchi zilizoendelea zinategemea kodi za wananchi wake kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na ziada kusaidia nchi maskini ambapo amesema baadhi ya miradi ambayo imeanza kutekelezwa kutokana na kodi za wananchi ni pamoja na ununuzi wa  ndege mpya,wanafunzi kusoma bure .

Amesema katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na muamko wa kulipa  kodi bila kulazimishwa tayari  mamlaka hiyo imeanza utaratibu wa kutoa elimu katika shule za sekondari na vyuo vikuu hapa nchini.

Nao baadhi ya wadau wa elimu wanasema ni vema serikali ikaanzisha mtaala wa elimu ya mlipa kodi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuwa na taifa lenye watu wenye uelewa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.






EmoticonEmoticon