Safina Sarwatt, Moshi.
BEI ya zao la Kahawa imedaiwa kuongeza kutoka dola za kimarekani 2.5
kwa kilo moja na kufika dola tatu (3) na kwamba mwaka 2020/2021
uzalishaji wa zao utaongezeka na kufika 150,000.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) Prim
Kimario alisema kuwa huenda matumaini ya ongezeko la thamani ya zao la
Kahawa ikaongezeka miaka mitano ijayo kutokana na takwimu
zinazoonyesha kuwa unywaji wa kinywaji cha kahawa nchini kipo kati ya
asilimia 5 hadi 7.
Akizungumza katika siku ya unywaji wa Kahawa duniani, kwenye viwanja
vya bodi hiyo mjini moshi, alisema kuwa hadi kufikia mwaka 2021
kiwango cha uzalishaji wa Kahawa kitaongezeka nakufikia asilimia 15.
Amesema kwamba kiwango hicho kinabainisha dhahiri kwamba watu wengi
hususani watanzania hawajui faida ya kutumia kinywaji cha Kahawa
ambacho ni kiburudisho kama vilivyo viburudishoa vingine.
Hata hivyo amesema kuwa utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti wa
Kahawa Tanzania TaCRI, unaonyesha kuwa mkulima atapata faida endapo
atakuwa na miche miatano ya Kahawa vinginevyo atabaki kulalama kuwa
zao hilo halina faida.
Pia alibainisha kuwa suala la mila na desturi kwa mkoa huu ni
changamoto ya kuzorota kwa zao hilo kutokana na maeneo mengi
yaliyokuwa yakilimwa kahawa kugawiwa kwa familia kama sehemu ya
kuendeleza makazi na maziko.
EmoticonEmoticon