MVUA YAZUIA MECHI YA MAN CITY VS BORUSSIA MONCHENGLADBACH



Mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Manchester City na Borussia Monchengladbach umeahirishwa mpaka leo Jumatano saa 3:45 za usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo zinaelezwa kuwa ni uwanja kujaa maji kupitiliza kufuatia mvua kubwa iliyoambana na radi kubwa yenye mwanga mkali kunyesha uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Man City, kuahirishwa huko kunatokana na sababu za kiusalama.

Tiketi zilizokatwa kwaajili ya mchezo huo uliopaswa kufanyika usiku wa kuamkia leo bado ni halali.

Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa Monchengladbach walitaka mchezo wao uchezwe saa 2:00 za usiku lakini Man City wamedai hakutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Upande mmoja wa goli katika uwanja huo ndiyo ulionekana kuharibiwa zaidi na maji. Mvua hiyo imesababisha hadi hitilafu kwenye mfumo wa kielectroniki.

Mwamuzi Bjorn Kuipers wa wenzake waliufanyia uchunguzi uwanja majira ya saa 2:55 za usiku lakini baadaye baada ya dakika 30 wakatoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo.


EmoticonEmoticon