SERENGETI BOYS YAIVA KUIKABILI CONGO BRAZAVILLE TAIFA SEPT 18


 

TIMU ya taifa ya vijana wa Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanya kambi yake kwa mafanikio huko mjini Victoria kwenye Kisiwa cha Mahe, nchini Shelisheli baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya dhidi ya Northern Dynamo.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili kutokana na kushambuliaana mara kwa mara.



Serengeti Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi watano, wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo inaondoka jioni ya leo Septemba 13, 2016 saa 11:00 jioni na ikitarajiwa kuingia nchini usiku wa saa 7:45 Septemba 14, 2016 ambako itakuwa kambini hadi siku ya mchezo Jumapili Septemba 18, mwaka huu.


Mchezo huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili, 2017.




EmoticonEmoticon