MKUU WA CHAMA CHA SOKA NCHINI SLOVENIA AZIBA NAFASI YA PLATINI UEFA


Aleksander Ceferin amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (Uefa).

Ceferin, ambaye ni mkuu wa Chama cha Soka nchini Slovenia, amepata kura 42 kwenye mkutano maalum uliofanyika jijini Athens nchini Ugiriki, idadi ya kura 29 zaidi ya mshindani wake Mdachi Michael van Praag.

Mslovenia huyo (48), anachukua mikoba iliyoachwa wazi na rais wa zamani wa shirikisho hilo Mfaransa Michel Platini, ambaye alijiuzulu baada ya kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka mwaka jana.

Ceferin ataziba nafasi hiyo ya Platini mpaka mwaka 2019 uchaguzi mwingine utakapoitishwa.


EmoticonEmoticon