DKT.RAMADHANI DAU AAPISHWA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ramadhani Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam.


Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.


Walioapishwa ni  kwanza, Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Pili, Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Adoh Stephen Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Adoh Mapunda kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.


Tatu, Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Tixon Nzunda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Baada ya kuapishwa, Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu Tawala wote watatu wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais Magufuli.


EmoticonEmoticon