MACHAVA YACHEZEA KICHAPO KOMBE LA MKOMBOZI


Safina Sarwatt,Moshi,

JUMLA ya timu nne zinashiriki mashindano ya mkombozi Cup ambayo yameanza kutimua vumbi jana katika viwanja vya Mandela mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Timu zinazoshiriki ni pamoja na shimatunda ,Machava ,New Generation na Kitayosec .
Lengo mashindano hayo ni kumbukumbu ya kumuenzi aliyekuwa mkurungenzi wa kituo cha mkombozi marehemu mama Mshana.

Katika mchezo wa kufungua dimba timu ya soka ya Machava imeshindwa kutamba mbele ya timu ya Shirimatunda baada ya kukubaliana na kipigo cha bao moja kwa sufuri .

Bao la washindi limepachikwa na mchezaji Hamad Rajab kunako dakika 19 ya kipindi cha kwanza baada ya kupiga mkwaju uliomshinda mlinda mlango wa timu ya Machava Fc Matayo Mayunga na mpira kuingia kimiani.

Mashindano hayo yanatarajia kuendelea tena leo kwa mchezo utakaozikutanisha timu za New Generation na Kitayosec inayojiandaa na ligi daraja la pili


EmoticonEmoticon