MENEJA wa klabu ya
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekanusha kuwa timu yake iko katika
mgogoro baada ya kupata vipigo katika mechi tatu mfululizo. Dortmund
walianza na kipigo cha kushtusha kutoka kwa Wolfburg na baadae
kuporomoka kwa alama saba mbele ya vinara wa Bundesliga Bayern Munich
kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa mahasimu wao hao huku
wakifungwa bao 1-0 nyumbani na Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa
barani Ulaya. Hata hivyo, Klopp amesisitiza kuwa wachezaji wake
hawajaathiriwa chochote na vipigo hivyo mfululizo huku akitegemea
kikosi chake kurejesha makali na kushinda katika mchezo wao dhidi ya
Napoli baadae leo. Klopp amesema pamoja na timu yake kutofanya vyema
katika mechi tatu zilizopita anaamini wachezaji wake watarejesha morali
iliyopotea haswa ikizingatiwa wametoka kuzitumikia timu zao za taifa na
wengine wameshinda katika mechi zao. Kwasasa Dortmund wanashika nafasi
ya tatu katika kundi F wakiwa na alama tatu nyuma ya Arsenal na Napoli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon