MASHINDANO ya langalanga
ya Bahrain Grand Prix mwakani ayanatarajiwa kufanyika usiku ili
kusheherekea miaka 10 ya mashindano hayo nchini humo. Waandaaji wa
mashindano hayo hivi wako katika pilikapilika za kufunga mfumo mpya wa
taa ili mashindano hayo yaweze kufanyika kwa ufanisi na mafanikio. Ofisa
Mkuu wa mashindano hayo nchini Bahrain Sheikh Salman bin Is Al-Khalida
amesema hakuna njia nzuri zaidi ya kusherekea miaka 10 zaidi ya kufanya
madereva washindane usiku. Bahrain itakuwa nchi ya pili kuandaa michuano
hiyo usiku huku Singapore wao wakiwa wa kwanza kwa kuandaa mashindano
hayo usiku toka mwaka 2008.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon