VIJANA WA SELEMANI MATOLA WAGARAGAZA MTENDELE YA ZANZIBAR


Timu ya Wekundu wa Msimbazi ya vijana leo imefanikiwa kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Mtendele kutoka Zanzibar kwa jumla ya goli 2-0 katika mashindano BancABC Super 8.

Magoli yote ya Simba yaliwekwa wavuni na EDUARD CHRISTOPHER ambaye alikuwa mwiba wa mchezo kwani aliwasumbua sana Wachezaji wa Timu ya Mtendele.

Kwa upande wake Kocha wa vijana hao wa Simba Seleman Matola amesema amefurahishwa na ushindi huo ila anaulalamikia uwanja ulikuwa mbovu ndio maana wakaibuka na ushindi mdogo wa goli 2.

Naye kocha wa Timu ya Mtendele amewalaumu waamuzi wa mtanange huo hasa mwamuzi wa kati kwa kudai kuwa alikuwa anawapendelea vijana wa Simba,hivyo wao kila wanapojaribu kufika langoni mwa Simba mwamuzi alipuliza kipenga kwa kudai ni off side.

Baada ya ushindi wa leo kwa vijana wa Simba sasa wanaelekea Mwanza kuumana na timu ya Jamhuri nayo ya Zanzibar hiyo siku ya Jumamosi.


EmoticonEmoticon