Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania inayotarajiwa kuanza September 15.
Hii
itakuwa mechi ya pili ya kirafiki ya Simba kucheza jijini Arusha baada
ya ile ya juzi dhidi ya Mathare United ya Kenya, ambao Wekundu hao wa
Msimbazi walishinda mabao 2-1.
Oljoro
JKT imetoka kwenye michuano ya timu za majeshi hapa nchini ambapo
ilichukua nafasi ya kwanza pamoja na Ruvu JKT na inacheza mechi hiyo
ikitokea Tanga ambako ilifungwa bao 1-0 na Coastal Union kwenye uwanja
wa Mkwakwani, Jumatatu.
Akizungumzia
pambano hilo Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovick amesema
atatoa nafasi kwa wachezaji wengi kwa kadri itakavyowezekana kwenye
pambano la leo.
Viingilio vitakuwa ni Sh 5,000 kwa VIP A, Sh 3,000 kwa VIP B na Sh 2000 kwa VIP C. Kiingilio kwa watoto kitakuwa ni Sh 1000.
Katika
mchezo, Simba itamkosa mshambuliaji wake Mzambia, Felix Sunzu ambaye
ameondoka nchini jana kuelekea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) kuhudhuria mazishi ya dada yake ambaye alifariki dunia juzi
jioni nchini humo.
Dada
huyo wa mshambuliaji huyo, alipatwa na mauti hayo akiwa amekwenda
kumtembelea ndugu yao, beki Stopila, anayechezea Tout Puissant Mazembe
siku sita zilizopita, kufuatia kupatwa na ugonjwa wa Malaria ulimpanda
kichwani (Cerebral Malaria).
Simba inatarajiwa kumenyana na Azam FC katika mechi ya kuwania
Ngao
ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kihistoria
hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili
kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba
na Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao
2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya
Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao
kihistoria.
Katika
mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi
Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka
jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga
Yanga mabao 2-0.
MABINGWA WA MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga
EmoticonEmoticon