Msemo wa kulia Ngassa kushoto Okwi kati Akufo kule Boban ulitawala sana katika vichwa vya mashabiki wa Simba SC, ambapo jana wameanza vyema msimu baada ya kila mshambuliaji kutoka na goli lake hiyo jana.
Simba SC waliwakabili African lyon ya Mbagala katika uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuwachapa Lyon goli 3-0, ikiwa ni clean shiti ya kwanza baada ya kufanya hivyo katika michuano ya Kagame Cup.
Alikuwa Emanuel Okwi katika dakika ya 33 kuwanyanyuwa mashabiki wa Simba SC, kabla ya kukaa kimya pale Mwinyi Kazimoto alipo ushika mpira katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru kupigwa penati iliyopanguliwa na Juma Kaseja katika dakika 35.
Wakati Lyon wakishanga Mrisho Ngassa aliumalizia mpira wa Said Cholo katika dakika ya 36 na kuiandikia Simba goli la pili na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Katika dakika ya 57 Emanuel Okwi aliangushwa katika eneo la hatari na Daniel Akuffo akiifungia goli la 3 Simba SC kwa Mkwaju wa penati na kumaliza mchezo kwa simba kushinda goli 3-0.
AZAM WAPATA USHINDI KWA MARA YA KWANZA KAITABA
Goli hilo pekee la Azam FC lilifungwa na Abdulhalim Homoud katika dakika ya 57, katika mchezo uliokuwa wa pande zote mbili.
YANGA VS PRISONS
Safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyo onyesha makali katika michuano ya Kagame na michezo ya kirafiki jana wameshindwa kuziona nyavu za Prisons ya Mbeya.
COASTAL VS MGAMBO
Baada ya kufanya vibaya katika michezo ya kirafiki, Coastal Union imeanza vyema ligi kuu baada ya kuwachapa goli 1-0 wageni wa ligi kuu Mgambo JKT.
Goli la coastal limefungwa na Jerry Santo katika kipindi cha pili.
MATOKEO MENGINE
COASTAL UNION 1-0 MGAMBO SHOOTING
PRISONS 0-0 YANGA
AZAM FC 1-0 KAGERA SUGAR
SIMBA SC 3-0 AFRICAN LYON
POLISI MORO 0-0 MTIBWA SUGAR
JKT RUVU 2-1 RUVU SHOOTING
TOTO AFRICAN 1-1 JKT OLJORO
EmoticonEmoticon