Twiga Stars wanaitaji ushindi wa 1-0 katika mchezo huo, baada ya kukubali kichapo cha goli 2-1 katika mchezo uliochezwa wiki 3 zilizopita katika jiji la Adis Ababa Ethiopia.
Kurejea kwa nahodha Sophia Mwasikile anaecheza soka katika nchi ya Uturuki, kunaimarisha safu ya ulinzi wa kikosi hicho ambacho kilicheza bila ya nahodha huyo katika mchezo wa awali, baada ya kunyimwa ruhusa na klabu yake.
Kwa ujumla kikosi cha Twiga stars kipo teyari kwa mchezo huo unaotaraji kuwa mgumu kwa pande zote mbili, kutokana na historia waliyonayo vinara hao wa soka la wanawake kwa ukanda huu wa CECAFA.
MOZAMBIQUE Vs TAIFA STARS
Katika mchezo wa awali uliochezwa mwezi wa pili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, hivyo kupelekea kusaka ushindi wowote ule jijini Maputo hapo jumapili.
Kikosi kilicho wamaliza Gabon wikend iliyopita ndicho hicho hicho kitakacho kuwepo jijini Maputo kusaka ushindi huo muhimu. Na endapo stars watashinda mchezo huo watasonga mbele kwenye hatua ya mwisho ya kusaka tiketi kw kucheza na moja ya timu iliyoshiriki mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.
Stars wamekuwa na wakati mgumu jijini Maputo kila wanapoenda kuvaana na timu ya taifa hilo na mara ya mwisho kwenda ilikuwa chini ya Jan Poulsein ambapo iliambulia kichapo.
EmoticonEmoticon