MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia
kufanyika kesho katika ukumbi wa Panandi Panandi uliopo Ilala, jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kocha wa Ngumi, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema, vijana wengi wamejitokeza kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.
Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo kuwa ni Ibrahim Class atakayezichapa na Twalibu, Mussa Sunga atazidunda na Ally Muhulo, Charo Issa atavaana na Shabani Kaoneka, Dickson Tembo na Raymon Mbwango huku Hassan Mijugu atapimana ubavu na Saidi Ally.
“Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti, vijana wengi wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wa mchezo wa masumbwi kufanikisha mashindano haya yaliyoandaliwa na Kinyogoli Foundation kwa ajili ya kuwapanga katika viwango mbalimbali vya ubora wachezaji,” alisema Super D
Alitaja baadhi ya mahitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji wakati wakiwa ulingoni, zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na dawa mbalimbali zitakazotumika kwa ajili ya kuwapa mabondia huduma ya kwanza.

EmoticonEmoticon