STARS WAJITITIMUA KWA IVORY COAST NA KUKUBALI KICHAPO CHA GOLI 2 UGENINI

Timu ya Taifa, Taifa Stars wamefungwa goli 2-0 na Ivory Coast katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili.


Katika mchezo huo uliochezwa jijini Abidjan nchini Ivory coasta, ulishuhudia wenyeji Ivory Coast wakipata goli katika dakika ya 18 kupitia kwa Kalou kabla ya Didier Drogba kufunga goli la pili katika kipindi cha pili kunako dakika ya 86.

Katika mchezo huo Stars walipoteza nafasi kadhaa ya kujipatia magoli na kuambulia kutoka matupu katika mchezo huo.


EmoticonEmoticon