KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Salum Machaku huenda akatolewa
kwa mkopo kwa nusu msimu kwa klabu yoyote kwenda kujifunza adabu kabla ya kurudishwa Wekundu wa Msimbazi.
Habari ambazo zimepatikana kutoka ndani
ya Simba, zimesema kwamba Machaku amekuwa akijisikia mno baada ya kufanya
vizuri msimu huu akiwa na jezi ya Wekundu wa Msimbazi kiasi cha kudharau hata viongozi wa timu hiyo.
Naye kiongozi mmoja wa juu wa timu hiyo, amesema kwamba uongozi ulifanya jitihada kubwa za kumbadili
kitabia Machaku, ikiwemo kumuweka chini ya mchezaji anayeogopwa na wachezaji
wote, Haruna Moshi ‘Boban’, lakini ikashindikana.
Kwa tetesi zilizopo,Salum Machaku ni kati ya wachezaji ambao wamo
kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na mahasimu wa jadi wa Simba,Yanga na katika
siku za hivi karibuni, Machaku amekuwa karibu mno na kipa wa Yanga, Shaaban Hassan Kado
ambaye waliwahi kucheza naye pamoja Mtibwa Sugar na timu ya taifa.
EmoticonEmoticon