Juma Jabu mwenye jezi nyekundu
BEKI wa kushoto wa Wekundu wa
Msimbazi Simba, Juma Jabu amesema yuko tayari kwenda Yanga au klabu nyingine
yoyote itakayoonyesha nia ya kumsajili kwa sababu anajali maslahi yake.
Kauli hiyo ya Jabu imekuja siku moja baada ya kuzagaa tetesi kwamba anataka kujiunga na Yanga pamoja na wenzake Juma Nyoso na Uhuru Selemani waliomaliza mikataba yao ya kuitumikia klabu bingwa ya Tanzania msimu wa 2011-2012 Simba.
Akizungumza jana na gazeti hili, Jabu alisema mkataba wake na Simba umekwisha na haoni dalili yoyote ya kuendelea kucheza hapo msimu ujao, hivyo yupo tayari kwenda timu yoyote itakayojali maslahi yake na kiwango chake uwanjani.
Hata hivyo uongozi wa Simba ulipoulizwa kuhusu suala la kuachana na nyota huyo walidai kwa sasa hawapo tayari kusema lolote hadi muda utakapofika.
Mwishoni mwa usajili wa msimu uliopita Simba iliingia kwenye mgongano na Jabu pamoja na Meshack Abel baada ya kuamua kuwatoa kwa mkopo katika klabu za African Lyon na Moro United.
Uamuzi huo wa Simba ulipingwa na wachezaji hao na baadaye uongozi wa mabingwa hao ulikubali Jabu kurudi kikosini huku Abel akivunja mkataba na kukaa nje ya uwanja kwa miezi sita.

EmoticonEmoticon