Kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings
Committee) ambacho kilikaa jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA
iliridhishwa na viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa
watawaangalia kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili
kuwaongeza katika orodha ya viwango.
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na
Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika
orodha ya viwango bora vya mabondia.
Mabondia hawa ambao watakuwa
miongoni mwa mabondia 15 bora duniani katika uzito wao ni,Francis Miyeyusho,
Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal Bruno
na Francis Cheka.
Ngowi aliwapendekeza
pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika ya Kusini, Namibia,
Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana, Nigeria, Morocco, Cameroon,
Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na Jordan.
Hii ina maana kuwa mabondia hao
waliowekwa kwenye orodha ya viwango vya IBF vya mabara wanaweza kupigania
ubingwa wa IBF wa Afrika na mabara wakati wowote.
Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba
ya Uajemi iliwakilishwa kwenye kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka
Tanzania, Katika vikao hivi vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu
wa IBF wanaohudhuria peke yao.
EmoticonEmoticon