Kampuni ya Arusha Art Limited wakala wa kuuza magari aina
Mercedes-Benz, Nissan na Suzuki kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na kampuni
ya uuzaji na usambazaji wa magari mapya ya Alliance Autos Tanzania Ltd ya
Tanzania imezindua gari mpya aina ya Volkswagen Amarok pickup katika viwanja
vya Magereza katika maonyesho ya Karibu Travel and Tourism Fair yanayoendelea
jijini Arusha.
Akiongea na Waandishi wa habari uwanjani hapo wakati wa
uzinduzi wa gari hilo Meneja Biashara wa kampuni Alliance Autos Tanzania Ltd
Tanzania ya kutoka jijini Dar es Salaam Alfred Minja alisema gari hilo ni imara
kwa matumizi ya barabara za nchini Tanzania na Afika Mashariki.
Minja alidokeza kuwa gari hilo limetengenezwa kutoka nchini
Ujerumani na ni mara ya kwanza kwa gari hilo kufika nchini na kuzinduliwa
jijini Arusha kwa mara ya kwanza ingawa litazinduliwa jijini Dar es Salaam
mwezi ujao.
“Gari hili Volkswagen Amarok pickup ni madhubuti kwa
barabara za Tanzania na limetengenezwa kukidhi mahitaji ya wananchi wa Tanzania
na kutokana na barabara zetu nyingi siyo imara hivyo hili gari litamudu katika
majira yote yawe ya mvua au kiangazi” alimesa Minja.
Minja aliwahimiza Watanzania kutumia gari hilo kwa kuwa
dhamani yake na uimara wake vinaendana na matumizi yake ya mafuta ni mazuri
kulinganisha magari mengine aina hiyo kutoka kampuni zingine za magari.
Alliance Autos Tanzania Ltd ni kampuni dada na kampuni ya CFAO Motors ya jijini
Dar es Salaam.
Kampuni ya Arusha Art Limited ya jijini Arusha ambayo ni
kampuni ya kuuza magari aina Mercedes-Benz, Nissan na Suzuki ndiyo itakuwa
wakala wa kuuza gari hilo aina Volkswagen Amarok pickup katika mikoa ya kanda
ya Kaskazini.
EmoticonEmoticon