NDUGU
wanahabari na mashabiki wa soka,
Nimechukua
fomu mbili za kuwania uongozi ndani ya
Klabu yetu ya Yanga, moja ni ya kuwania Makamu Mwenyekiti na nyingine ikiwa ni
kuwania nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
Nimelazimika
kuchukua fomu za nafasi hizo mbili ili kuwaachia wanachama wa Yanga kunipima na kuona ni katika nafasi ipi
wanaona naweza kuwatumikia ipasavyo ili kuiletea Klabu yetu mafanikio zaidi kuliko ilivyo sasa.
Nina
uzoefu mkubwa katika uongozi kwa tasnia zote kuanzia michezo, siasa, biashara
na masuala mengine yanayoizunguka jamii.
Uzoefu katika michezo unatokana na ushiriki wangu katika masuala kadhaa
yanayoihusu Yanga yenyewe na michezo mingine kadhaa.
Ushiriki
wangu kwa Yanga umekuwa unaufanya
uongozi wa Yanga kwa vipindi tofauti kunishirikisha katika baadhi ya masuala
yanayoihusu Klabu.
Ni
hatua hiyo ndiyo iliyowezesha uongozi wa Yanga
mwaka jana kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Ushindi hatua iliyoiwezesha Timu kutwaa Ubingwa wa
Bara. Nimekuwa pia nikisaidia wachezaji wa zamani wa Yanga (Yanga Veterans)
kushiriki katika michezo mbalimbali ili kuendelea kuimarisha afya zao baada ya
kustaafu soka.
Kisiasa
nimewahi kuwa Mbunge wa Njombe Magharibi, nafasi ambayo iliniwezesha kuzisaidia
timu kadhaa za michezo ikiwemo Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake (Twiga Stars)
na Yanga yenyewe.Katika hatua nyingine ya kuthamini michezo kupitia nafasi
yangu kama Mwenyekiti wa Kampuni ya Yono Auction Mart nilianzisha timu ya Soka
ya Yono ambayo imekuwa ikishiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya
nchi, sababu zinazothibitisha kwamba nimekuwa jirani na soka kwa muda mrefu
sasa.
LENGO
KUU
Nimeshawishika
kuwania uongozi ndani ya Yanga nikiwa na Kauli Mbiu ya ‘Maslahi ya Wachezaji
Kwanza’, kauli mbiu yenye lengo la kuboresha maslahi kwa wachezaji wa Yanga ili
kuinua kiwango cha soka letu na hivyo
kutamba katika michezo ya ndani na nje ya nchi.
Nikichaguliwa
kuingia katika uongozi wa Yanga nitashirikiana na viongozi wenzangu katika
kuvunja makundi ili kuwezesha kuwa na Yanga Moja Imara itakayotuvusha kutoka
katika soka la sasa lisilo na tija hadi katika soka la kisasa lenye mafanikio
kwa Klabu, Wachezaji na Wanachama wote.
Nimejitupa
katika kuwania uongozi ndani ya Yanga
bila kuwa na ajenda ya siri. Baadhi ya wanaYanga wamekuwa wakijitokeza
kuwania uongozi wakiwa na ajenda za kutaka kujinufaisha wao binafsi badala ya
klabu na wachezaji.
Yanga
inaweza kuwa Timu Bora na Imara tofauti
na sasa kama itapata viongozi watakaoimarisha
matawi ya Klabu ambayo mengi yanasuasua na pia atakayeweza kubuni vyanzo vipya
vya mapato na kusimamia vile vilivyopo kama majengo na vinginevyo kwa kuthubutu
na kujiamini, sifa ambazo mimi ninazo.
Naamini
kwa pamoja tutajenga Yanga Bora na Yanga Imara.
YONO
STANLEY KEVELA
EmoticonEmoticon