Napenda
kuwajulisha wanamabadiliko kuwa kuanzia jumapili tarehe 10 mwezi
huu,saa tatu na nusu usiku nitaanza kurusha mfululizo wa vipindi vyangu
TBC.
Lengo la vipindi hivi ni kuonyesha kazi mbalimbali zilizofanywa na
serikali kwa kushirikiana na taasisi ya mkapa foundation haswa katika
masuala ya afya.
Vipindi
pia vitaonyesha changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo katika sekta
ya afya ili kwa pamoja tuweze kuzitatua haswa katika maeneo ya
pembezoni mwa nchi(vijijini).
Vipindi hivi nimefanya mwenyewe na kampuni binafsi na vitarushwa TBC kwa ufadhili wa mkapa foundation.
Napenda ieleweke,mimi jerry muro sijaajiriwa TBC bali narusha vipindi vyangu pale kwa muda wa miezi miwili na nusu.
Mashabiki
na wapenzi wa kazi zangu karibu tutazame ili pamoja tuweze kukabiliana
na changamoto zinazolikumba taifa letu na hatimae tuweze kuleta maisha
bora kwa kila Mtanzania.
EmoticonEmoticon