Mabingwa wa Tanzania wekundu wa
Msimbazi Simba SC wametangaza bei ya mshambuliaji wao hatari na mfumania nyavu
EMMANUEL OKWI kwa timu yoyote inayomtaka kwa kufuata masharti.
Akizungumza na SUNRISE RADIO
mapema leo msemaji wa mabingwa hao,EZEKIEL KAMAGWA amesema kuwa kwa timu yeyote ile
inayomtaka mshambuliaji wao huyo wawe tayari kutenga kiasi cha shilingi EURO
850,000/= ambayo ni sawa na shilingi bilioni mbili za kitanzania.
KAMWAGA amesema wamepata ombi
kutoka nchini AUSTRIA ya mawakala wanamlilia kutaka kumpeleka nchini humo
kusakata kabumbu hivyo wamewaambia kama wanaweza kulipa BILIONI 2 za Kitanzania
watamchukua OKWI.
Mawakala hao wamesema kwa sasa
wanatafakari kumnunua mchezaji huyo kwani ana kiwango cha hali ya juu hasa
katika kupachika mabao hivyo atawafaa katika timu yao na wanafikiria dau hilo
waliloambiwa na Uongozi wa mabingwa hao.
Pia amesema kama klabu inamhitaji
OKWI lazima ifuate masharti matatu ambayo ni MAISHA MAZURI KWA
WACHEZAJI,MISHAHARA na UONGOZI BORA.
KAMAGWA amesma timu za YANGA na AZAM zimeshindwa kufikia dau
hilo na kuitaka YANGA kufanya uchaguzi ndo waje kuongea na Uongozi wa Simba
kwani YANGA kwa sasa hawana uongozi hivyo kutokana na masharti hayo
waliyoyataja.
KAMWAGA ameendelea kusema kuwa
wameweka dau hilo kwa OKWI kwani ana uwezo mkubwa kisoka na angekuwa Ulaya
thamani yake ingekuwa mara tatu au nne
kwa dau walilotoa hivi sasa.
EmoticonEmoticon