WAZEE WA YANGA WASEMA MADENI YA PAPIC NA WACHEZAJI CHANZO CHA KUPIGWA 5-0 NA SIMBA


  
Baada ya kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Tanzania bara na mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na kati katika michuano ya kimataifa,Wekundu wa Msimbazi Simba na  kuifanyia mauaji ya kutisha Watani wao wa jadi Yanga ambayo ni klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati kwa kuifunga jumla ya goli 5-0,Wazee wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Akilimali Ibrahimu, umeweka wazi kilichopelekea timu yao kupokea kipigo kutoka kwa Watani wao wa jadi. 

Mzee Akilimali amesema timu ya Yanga iliingia kambini siku tatu kabla ya mchezo dhidi ya Simba huku wachezaji wakiwa hawana morali yoyote kutokana na kuwa walikuwa wakidai malimbikizo ya mishahara na bonasi za mechi za msimu mzima wa ligi kuu ya Vodacom.

Akilimali ameendelea kusema kuwa kwa muda mrefu kocha mkuu wa Yanga amekuwa akidai uongozi  shilingi milioni 24 za malimbikizo ya mshahara wake, hali iliyopelekea Papic kutokuweza kuishi vizuri hivyo kupelekea kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi.
Pia mzee Akilimali amesema madai ya bonsai kwa wanandinga hao ya shilingi 70,000 kwa kila mchezo umechangia timu kufungwa dhidi ya Simba,lakini katika hali ya kushangaza ndani ya kipindi chote cha Ligi kuu ya Tanzania bara uongozi wa Yanga ukiongozwa na Nchunga haukuwalipa wachezaji bonasi za mechi zote za msimu kama walivyokubaliana.
 Akilimali amesema hali ya kambi ilikuwa hairidhishi kifedha na kuwafanya wachezaji  kutokuwa katika hali nzuri ya kiakili kuweza kupambana na watani wao wa jadi na kuambulia kipigo kama kile mbele ya mashabiki wao.


EmoticonEmoticon