Baada ya kumaliza Ligi Kuu bara kwa
kishindo, Simba sasa inajipanga kwa safari ya kwenda Sudan kwa ajili ya mechi
ya michuano ya kimataifa, na imepanga kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi.
Akizungumzia safari hiyo, makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kuwa timu yao itaondoka kesho kwa ndege ya kukodi kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya michuano hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa takriban wiki moja iliyopita, Simba ilishinda kwa mabao 3-0 na hivyo inahitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kwenye mechi hiyo ili kufuzu kwa hatua inayofuata.
Naye Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa mafanikio ya
timu yao msimu huu yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya uongozi wa sasa, uongozi uliopita na marafiki wa klabu hiyo ‘Friends of Simba’.
Rage ameyazungumza hayo baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Yanga, na kusema kuwa mshikamano
uliokuwepo ndani ya klabu hiyo kwa sasa ndio siri ya mafanikio ya timu yao.
Rage amesema kuwa siku zote panapokosekana mshikamano madhubuti miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo lazima timu yao inakuwa haifanyi vizuri, lakini kwa sasa kwa kuwa wako pamoja ndio maana mafanikio yanaonekana

EmoticonEmoticon