LICHA YA HUJMA TP MAZEMBE YAFUZU HATUA YA MAKUNDI



Timu ya Tp Mazembe ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imetinga hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 na El Merrekh ya Sudan hapo jana usiku.


Tp Mazembe hapo jana usiku ilitoka sare hiyo kwenye mchezo wa marudiano baada ya ushindi wa mabao 2-0 mjini Lubumbashi majuma mawili yaliyopita na hiyo jana kuonyesha uma wa wapenda kabumbu kuwa wao bado wanastahili kuitwa mabingwa wa Afrika.

Tp Mazembe licha ya kufanyiwa hujma na El Merrekh kwa basi lao kupigwa risasi wakiwa Sudan lakini wanastahili pongezi kwa kutoa sare ya bao 1-1 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.


Baada ya Tp Mazembe kufanikiwa kusonga mbele hiyo jana usiku,leo usiku ni zamu ya wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na kati waliobaki Wekundu wa Msimbazi kupeperusha bendera ya Tanzania huko Sudan wakati wakimenyana na El Ahly Sand.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinatarajiwa kuwa kama kifuatavyo:


 
 1: Juma Kaseja

2: Shomari Kapombe

3: Amir Maftah

4: Victor Costa

5: Kelvin Yondan

6: Mwinyi Kazimoto

7:  Uhuru Seleman

8: Patrick Mafisango

9: Felix Sunzu

10: Haruna Moshi Boban

11:  Emmanuel Okwi

SUB:
Barthez, Juma Jabu, Derick Walulya, Machaku, Obadia.




EmoticonEmoticon