VIJANA WA TANZANIA VITANI LEO DHIDI YA VIJANA WA SUDANI


 
Ngorongoro Heroes kuikabili Sudan leo jumamosi kuanzia majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambayo itachezwa kwenye uwanja wa Khartoum Sudan.
 katika michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 20.

Mechi hiyo ya marudio ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 20 ambayo kwa mechi ya awali Ngorongoro Heroes iliikuba na ushindi wa goli 3 kwa 1.

Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo Afisa habari wa TFF Boniface Wambura ambaye yupo na timu Khartoum  amesema kikosi kinafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Omdurman kiko katika hali nzuri na kitatumia mfumo wa 4-4-2 kwa mujibu wa kocha wa kikosi hicho Kim Poulsen na amesema nia ya kutumia mfumo huo ni kwa lengo la kushambulia muda wote wa mchezo.

Wambura ameendelea kusema nyumbani tuliwafunga mabao 3-1, hivyo hapa watacheza kwa kushambulia tu huku na sisi tukizuia mashambulizi yao kwa kushambulia.

Kikosi cha Ngorongoro Heroes kinaundwa na; Aishi Manula, Jamal Mroki, Issa Rashid, Samir Ruhava, Dizana Ramadhan,Frank Damayo, Frank Sekule, Omega Seme, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva na Ramadhan Singano.
Wachezaji wa akiba ni Saleh Malande, Hassan Dilunga, Ramadhan Khamis, Said Zege, Jerome Lambele,
Emily Mugeta na Atupele Green.

Mtanange huo hautakuwa na kiingilio kwa washabiki watakao hudhuria itachezeshwa na Aden Abdi Djamal wa Djibouti,akisaidiana na Wadjibouti wenzake Egueh Yacin Hassan, Bogoreh Salime Fahan na Aden Ali Farah kamishna wa mchezo huo ni Patrick Naggi wa Kenya.

Ngorongoro Heroes itaanza safari ya kurejea nyumbani mara baada ya mechi hiyo, Itaondoka Khartoum saa 9 alfajiri kupitia Nairobi Kenya na kuwasili Dar es Salaam Jumapili saa 3.20 asubuhi.


EmoticonEmoticon