AZAM FC KULAMBA DUME MSIMU UJAO


Mchezaji raia wa Kenya George Blackberry Odhiambo ametua nchini hii leo kwa lengo la kufanya mazungumzo na klabu ya wanalambalamba Azam fc kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano mingine ya kimataifa.

Odhiambo Blackberry amerejea nchini Kenya kutoka Denmark alikokuwa anakipiga na timu ya Rangers Fc baada ya mkataba wake wa miaka minne kuvunjwa kwa makubaliano baina ya timu hiyo na Odhiambo.

Odhiambo kabla ya kuelekea nchini Denmark alikuwa anakipiga na klabu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo kwa hivi sasa habari zilizopo zinasema kuwa klabu hiyo inataka kumrudisha mchezaji huyo ila inasubiriwa kauli kutoka kwa kocha Logarusic


EmoticonEmoticon