CHELSEA YAPELEKA SALAMU KWA BAYERN MUNICH
Chelsea the Blues imetwaa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuifunga Liverpool kwa bao 2-1
Wafungaji wa mabao hayo kwa upande wa Chelsea ni Ramires na Didier Drogba walioifungia mabao hayo na kwa upande wa Liverpool bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Andy Carroll kwenye Uwanja wa Wembley.
Ramires alifunga bao la kwanza baada ya makosa ya Jay Spearing kabla ya Drogba kufunga la pili na Andy Carroll aliyetokea benchi kuifungia Liverpool bao la kufutia machozi kwa kutumia makosa ya John Terry.
Lakini Liverpool ni kama walinyimwa bao la kusawazisha na refa baada ya mpira uliopigwa na Carroll kuonekana kabisa umevuka mstari wa goli, lakini refa akachomoa.
Chelsea wamechukua kikombe hicho cha FA huku wakijiandaa kwa mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Ujerumani.
EmoticonEmoticon