Dionis Moyo-Mkurugenzi Sunrise Radio
Kituo cha radio jijini Arusha cha Sunrise Radio kimepewa tuzo ya kituo bora kwa mkoa wa Arusha na klabu ya Azam fc kwa ushirikiano walioonyesha kwenye ligi kuu ya Vodacom iliyomalizika juzi huku Simba wakiibuka mabingwa wa ligi hiyo ya Vodacom.
Akizungumza kwa njia ya simu na Ezra Agora wa Sunrise Radio,
Afisa habari wa Azam fc,Jaffari Iddi Maganga,amesema tuzo hiyo ya heshima
wameitoa kwa Sunrise Radio Arusha kwa ushirikiano walioonyesha kwa Azam fc
tangu mwanzo wa ligi kwa kuuliza kila kitu kinachoendelea klabuni hapo.
Ikiwa hiyo ni tuzo ya pili ya michezo Sunrise Radio wanapewa
tangu mwaka huu uanze baada ya ile waliyopewa na Chama cha soka Manispaa ya
Arusha mjini kwa kutangaza ligi ya Wilaya hiyo na pia wakitoa tuzo zingine kwa
wanamichezo wa radio hiyo ambao ni Ally Shemdoe ambaye ni mhariri wa michezo wa
Sunrise Radio na tuzo nyingine ilienda kwa Dionis Moyo ambaye ni Mkurugenzi
mtendaji wa kituo hicho.
Kwa upande wa Mhariri wa Michezo wa Sunrise Radio Ally Shemdoe
amesema kwamba wameipokea tuzo hiyo ya heshima waliyopewa na Azam fc kwani ni
kazi kubwa wameifanya kwenye mizunguko yote ya ligi kuu ya Vodacom.Pia amesema
siyo Azam pekee ndiyo walikuwa wanaifuatilia bali timu zote zilizokuwa
zinashiriki ligi kuu lakini Azam fc wameona mchango wao ndiyo maana wametoa
tuzo hiyo ya heshima kwa Sunrise Radio.
Shemdoe ameendelea kusema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano
kwa timu zote hapa nchini lengo likiwa ni kukuza michezo Tanzania ili
kufahamika kimataifa zaidi,pia ameviasa vyombo vingine vya habari kuonyesha
ushirikiano ili kufanikisha na kuinua michezo Tanzania.
Hivyo Sunrise Radio imemteua muandaaji wa vipindi(Producer)
Mussa Kinkaya kwenda jiji Dar siku ya Jumapili kwa ajili ya kuchukua tuzo hiyo
ya heshima waliyopewa na Azam fc ambayo inatolewa simu ya Jumatatu kwenye ofisi
za Azam jijini Dar.
Kwa upande wake Mussa Kinkaya amesema amefurahi Sunrise
Radio kupewa tuzo hiyo ya heshima na Azam fc kama muandaaji wa vipindi kwenye
kitengo hicho cha michezo.
Tuzo hizo zilitolewa na Azam fc siku ya Jumapili baada tu ya
kumalizika kwa ligi kuu na Azam kushika nafasi ya pili hivyo kuamua kufanya
sherehe ya kupongezana kwa mafanikio waliyoyapata kwa muda mfupi na kuahidi
kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania.
Mbali na Sunrise Radio kupewa tuzo hiyo vyombo vingine vya
habari vilivyopewa tuzo za heshima ni pamoja na TBC,Radio one na Mlimani zote
za jijini Dar.
Kila la kheri Mussa Kinkaya kwa safari ya kwenda Dar
kuchukua tuzo hiyo.
EmoticonEmoticon