Mwanamke
mmoja aitwaye Nuru mkazi wa Kwa Mrefu mkoani Arusha anatuhumiwa kumkata
vibaya kwa panga mume wake Edward John.
Tukio
hilo limetokea jana huku mashuhuda wakidai kuwa amefanya hivyo kumshinikiza
mume huyo kuacha tabia ya kutompa pesa za matumizi.
Taarifa
za tukio hilo zinasema kuwa jana majira ya saa nne usiku, wakati majirani
waliposikia kelele za kuomba msaada hivyo kuingia katika nyumba hiyo na kumkuta
bwana huyo akiwa ameloa damu.
Hali
ya Edward John bado ni mbaya, ingawa anaendelea kupatiwa matibabu katika
hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
EmoticonEmoticon