Joshua Nasari-Mbunge Arumeru Mashariki
JESHI la
Polisi limempa masaa machache Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua
Nassari na endapo kama hatajisalimisha kwa jeshi hilo basi nguvu zaidi
zitatumika katika kumsaka kwa kuwa Mbunge huyo ametoa lugha za uchochezi kwa
wananchi katika mkutano uliofanyika viwanja vya NMC ambao ulihudhuriwa na
viongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Akiongea na waandishi wa habariNaibu
Kamishna wa jeshi la Polisi hapa nchini Bw Isaya Mngulu amesema kuwa Mbunge huyo alitoa matamko hayo
katika viwanja vya NMC ambapo alidai kuwa Rais hapaswi kufika katika kanda ya
kaskazini hasa katika jimbo hilo endapo kama atashindwa kufuatilia sakata la
mauaji ya aliyekuwa kada wa Chadema kwa haraka sana
Aidha Mngulu
aliongeza kuwa mbali na mbunge huyo kusema maneno hayo pia aliwaambia
wananchi waliokuwa katika maeneo ya viwanja vya NMC kuwa yeye ndiye
atakayekuwa Rais wakati Waziri mkuu atakuwa ni Aliyekuwa Mbunge wa
Arusha Mjini Bw Goodbless Lema hali ambayo inaonesha kauli za uchochezi.
Akiongelea
sakata la baadhi ya wanachama wa Chadema kudai kuwa wanatishiwa kuuawa na watu
wasiojulikana kuwa madai hayo ni ya uongo na wanaotuma na kusambaza ujumbe
mfupi(SMS) ni makada wa Chadema na mpaka sasa Jeshi hilo limeshawabaini.
Awali alisema
kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuwatia Mbaroni
watu12 ambao walihusika na Mauaji mbalimbali katika eneo la Meru ambapo watu 3
wameshafikishwa mahakamani huku wengine wakiwa wanaendelea na uchunguzi
katika tukio la kuuawa vibaya kwa Kada wa Chadema wiki chache zilizopita.
Pia alisema
kuwa mbali na kuweza kuwashikilia watu hao 12 ambao wanahusika na mauaji
ya Kada wa Chadema pia bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi zaidi ili
kuweza kuwatia mbaroni pia waliohusika na mauaji ya bibi kizee Bi Martha
Joseph(77) kwa madai kuwa alikuwa ni mchawi katika eneo la Nkoaranga
EmoticonEmoticon