MKUU WA MKOA WA ARUSHA MAGESA MULONGO ATEMA CHECHE KWA WABQADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA


    •  

    • MKUU wa Mkoa wa Arusha Bw. Magessa Mulongo ametangaza rasmi kuwa wakurugenzi wote ambao halmashauri zao zitapata hati chafu, huo utakuwa ndiyo mwanzo na mwisho wa kazi zao.

      Tamko hilo alilitoa jana mkoani humo wakati akihutubia katika kilele cha sherehe za Siku Kuu ya Wafanyakazi ambayo hufanyika kila ifikapo Mei Mosi duniani kote.
    • Mei mosi hiyo mkoani hapa, mwaka huu ilifana vilivyo kutokana na idadi kubwa ya wakazi wa Jiji la Arusha yakiwemo magari ya maonesho kutoka mashirika mbalimbali, taasisi na vyuo vya msitu mkoani hapa yakishiriki huku kauli mbiu ya Mei Mosi ikiwa 'Mfumuko wa bei, kodi kubwa ni kitanzi kwa wafanyakazi'.

      Hata hivyo Bw. Mulongo aliwataka wakurugenzi wa halmashauri ambao wamepata hati chafu kujirekebisha mapema kwa kuwa watapoteza kazi na alibainisha kuwa
      hakuna masihara katika hilo kwani aliyekuwepo na asiye kuwemo atanasa katika
      mtego huo wa ubadhirifu wa mali za umma.

      Pia aliwataka wakurugenzi hao wakae katika Baraza la Madiwani na kuandaa bajeti endelevu kwa maslahi ya wananchi wa Jiji la Arusha ili kuondoa kero na manunguniko ya wananchi juu ya tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa
      katika halmashauri.
    •  
    • Mulongoamesema, kuwa kutokana na Kampuni ya Bayport kutoza riba kubwa kwa walimu hao ofisi yake inamtuma Mkuu wa Wilaya Bw. Raymond Mushi kulifanyia kazi suala
      hilo na kuwa DC amekabidhiwa rungu la kushughulikia jambo hilo.

      "Sisi wote ni serikali na ikija kwenye suala la ubadhirifu wa mali za umma tusiwanyooshee watu fulani vidole ila walaji ni wote pamoja na sisi wananchi, ubadhirifu una mtandao ndani ya halmashauri zetu kwa hiyo ubadhirifu huo ni wetu sote kwani tunashiriki kula fedha za umma bila kuhoji zinatokea wapi,”

      Aidha, alisema watahakikisha wanapiga vita kwa kuwa hilo ni jiji la wajanja na iweje halmashauri ipate hati chafu watu waendelee kukaa kimya.

      Wakati huo huo Kampuni ya A TO Z imekuwa mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa wakati TBL imekuwa mshindi wa kwanza kwa mashirika makubwa huku NCAA imekuwa mshindi wa kwanza kwa mashirika ya hifadhi ya wanyama na Banana Investment imekuwa mshindi wa kwanza kwa viwanda vidogovidogo Mkoa wa Arusha


EmoticonEmoticon