Uongozi wa Yanga umesema upo tayari kuwaachia
viungo wake wa kimataifa, Haruna Niyonzima ‘Niyo’ na Hamis Kiiza kuondoka
klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ikiwa klabu zinazowahitaji zitafikia
kiwango watakachohitaji.
Kumekuwa na taarifa kuwa viungo hao ambao
wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu, wapo katika mipango ya kwenda kucheza
soka nje ya Afrika, Niyonzima yeye anatarajiwa kutimkia Ulaya wakati Kiiza
anaweza kwenda Malaysia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum
Rupia, alisema wao hawawezi kumzuia mchezaji yeyote kuondoka kwenye klabu hiyo
na udai kuwa wanachoangalia ni maslahi mazuri ambayo yatafikiwa.
Rupia amesema licha ya wachezaji hao kuwa na
mkataba na Yanga mpaka mwishoni mwa msimu wa 2013/2014, lakini klabu yoyote
inayowahitaji wachezaji hao, inatakiwa kufanya mazungumzo na Yanga ili kufikia
makubaliano ya dau la usajili.
“ Rupia ameendela kusema hatuwezi kuwazuia Niyonzima na Kiiza kwenda
kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, wao soka ndiyo ajira yao, hizo klabu zinazowahitaji ni vema
zikafanya mazungumzo na viongozi wa Yanga.
“Bado ni wachezaji halali wa Yanga, mikataba yao inatarajiwa kumalizika msimu ujao wa 2013/2014,
hatukatai fedha, tukiwaachia akina Niyonzima na Kiiza tutasajili wengine,
wanaowataka bure wasubiri hadi mikataba yao
itakapomalizika.”
EmoticonEmoticon