Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika raundi ya
25 kesho (Aprili 28 mwaka huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera
Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa
African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Aprili 30 mwaka huu Azam na Toto African
zitacheza Chamazi wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5
mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa),
Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting
vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs
Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro),
Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es
Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri,
Morogoro).
EmoticonEmoticon