Kichanga kinachokaridiwa kuwa na siku moja kimekutwa kimetupwa katika migomba iliyopo mtaa wa shamsa jijini Arusha ambapo mama yake hajafahamika bado huku baadhi ya viungo vyake vikiliwa na mbwa usiku
Tukio hilo ambalo lilikuwa la kusikitisha lilitokea jana majira ya saa 12 asubuhi ambapo wakazi wa eneo la shams jijini hapa walimiminika kwenda kujionea kichanga hicho ambacho kilikuwa kimetelekezwa na mama yake huku kikiwa hakina baadhi ya viungo vya mwili wake
Wasamaria wema baada ya kukuta kichanga hicho hakina baadhi ya viuongo vya mwili wake walichukua hatua ya kukifunika na kanga na baadae kupiga simu polisi
Hata hivyo kwa mujibu wa mashuhuda walisema kuwa kichanga hicho kinakadiriwa kuwa cha siku moja na tayari alikuwa amekamilika kuwa mtoto.
“jamani huyu ni mtoto kabisa inaelekea mama yake alimzaa mzima akaamua kumnyonga na kumtupa hapa usiku halafu mbwa akampitia na kumla baadhi ya viungo vyake”alisema mama shuhuda ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aidha kichanga hicho kililiwa na mbwa sehemu ya mguu wake na sehemu za siri huku kikiwa kinamchubuko sehemu ya usoni.
Kichanga hicho ambacho kilikuwa cha kiume kilivuta hisia ya watu wengi huku watu wakitupa lawama kwa mama mzazi aliyefanya kitendo cha kinyama kuwa ni bora hata angemtupa hata mlangoni kwa mtu au ange mwacha hata hospitalini
“Namshangaa sana aliyefanya kitendo hichi hana hurama hata kidogo ni muuwaji na anastaili adhabu kubwa akipatikana ni bora hata angemwachia mtu,,kuna watu wanatafuta mtoto na hawapati”alisema Mama Miriam ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo
Hata hivyo mwandishi wetu alimtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Bw.Thobias Andengenye kudhibitisha tukio hilo simu yake iliita bila kupokelewa
Kutokana na kitendo hicho cha kinyama hadi sasa hajafahamika ni nani alishiriki kufanya hivyo kitendo hicho cha kutupa kichanga hicho.

EmoticonEmoticon