Msafiri Mbwambo alivyojinjwa
Mwenyekiti wa kata ya Usa River mkoani Arusha wa Chadema,Msafiri Mbwambo ameuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia leo.
Taarifa za tukio hilo la kikatili zimetolewa na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nasari wakati akizungumza na moja kwa moja na kituo cha Radio cha Sunrise radio Arusha toka eneo la tukio.
Nasari amesema kuwa wao kama wana chadema na wakazi wa Usa River wanalitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa kabla ya tukio hilo marehemu Mbwambo alikuwa na wenzake kwenye eneo la starehe huku yeye akiwa hanywi chochote,lakini ghafla alipigiwa simu na watu hao wakidai kuwa kulikuwa na wanachama wa ccm wanataka kurudisha kadi na kujiunga na Chadema.
Baada ya hapo marehemu Mbwambo alichukua pikipiki na kuwafuata watu hao,lakini hakurudi hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa kandokando ya barabara eneo la makaburi,huku pikipiki na vitu vingine alivyokuwa navyo vikibaki eneo la hilo bila kuchukuliwa na wauaji hao.
EmoticonEmoticon