MAUGO ADAI USHIRIKINA UMECHANGIA KUTUPA GLOVES DHIDI YA CHEKA

 
 Francis Cheka   



 
Mada Maugo                                                                                               

BONDIA tishio kwa hivi sasa nchini, Francis Cheka  kutoka mji kasoro bahari(Morogoro),amemtwanga mpinzani wake Mada Maugo kwa mara ya tatu mfululizo kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba katika pambano lililokuwa la raundi 12, kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba jijini Dar es Salaam.

Licha ya kushinda pambano hilo,Cheka amesema Maugo ni bondia mzuri sana na hakuna bondia mwenye makonde makali nchini kama Maugo licha ya kumtwanga.

Cheka ameendelea kusema anashukuru sana Maugo kuvua gloves kuelekea raundi ya saba kwakuwa Maugo alileta upinzani mkubwa sana na kumtia uoga kwenye pambano hilo la raundi 12.

Maugo baada ya kupigwa ngumi nyingi katika raundi tatu mfululizo, kiasi cha kutabiriwa kukaa chini wakati wowote,na hatimaye mwanzoni mwa raundi ya saba Mada Maugo hakurejea tena ulingoni.


Naye Bondia Karama Nyilawila ambaye alikuwa msaidizi wake kwenye pambano hilo alitupa taulo ulingoni akisema bondia wake hataendelea tena na pambano.


Refa John Shipanuka kutoka Zambia aliyelimudu pambano hilo, alimuinua mkono Francis Cheka na kumtangaza mshindi kwa TKO raundi ya saba.


Baada ya Cheka kutangazwa bingwa wa pambano hilo, Maugo Maugo aliinuka kwenye kona yake na kwenda kumkumbatia Cheka na kocha wake,huku akisema kwamba amesalimu amri baada ya kuishiwa pumzi.


Baada ya kuibuka mshindi, Cheka alisema kwamba anamshukuru Mwenyezi Mungu amemuwezesha kuendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania na sasa anageuzia makali yake kwa Japhet Kaseba ambaye naye ameomba pambano la marudiano na Cheka.


Katika pambano hilo, refa Shipanuka alimdhibiti Mada Maugo mwenye desturi ya kuwakumbatia wapinzani wake ili kukwepa kupigwa na pia kupumzikia kwenye miili yao na refa kufanikiwa kwa hilo.


Baada ya kuondoka ulingoni hapo nilimtafuta Mada nikamuuliza kwanini amevua gloves akasema alikuwa haoni wakati akipambana na Cheka na kumalizia kwamba pambano hilo lilikuwa na ushirikina.


Mada ameendelea kusema hatokataa kucheza pambano na Cheka kwakuwa maisha yake ni masumbwi hivyo anaweza kutangaza hatocheza na Cheka pambano lingine likatokea.


Kwa upande wake Cheka nilimuuliza juu ya tuhuma za ushirikina kwenye pambano hilo,amesema Maugo anamchafulia kwa mashabiki wake na kusema Maugo alikuwa anaongea sana kwenye vyombo vya habari,hivyo ni mtu mwenye maneno mengi na kusema hizo ni mbinu za kijitetea kwa washabiki wake.

Licha ya kupigwa ,Mada Maugo alilianza pambano hilo vizuri na katika raundi ya pili almanusra ashinde kwa Knockout (KO) baada ya kumkalisha mpinzani wake Cheka kwa ngumi kali iliyompeleka chini,lakini Cheka aliinuka na kuendelea na pambano,na baadaye raundi ya nne kuanza kuutawala mpambano huo.


Katika  mapambano ya utanguliz,Simba Watunduru alimpiga kwa KO raundi ya sita Mohamed Kashinde katika pambano la uzito wa Feather, wakati Amos Mwamakala alimpiga kwa pointi Said Muhiddin uzito wa Light.

Moro Best alimpiga Nassib Ramadhan kwa TKO raundi ya nne uzito wa Bantam na Salima Kabombora alimpiga Asha Ngedere kwa pointi uzito wa Bantam.

Licha ya kaka kumtwanga Mada Maugo,kwa upande wake mdogo wake Cheka, Cosmass Cheka alipigwa kwa pointi na Sadiki Momba katika pambano la uzito wa Light na Hajji Juma alimpiga kwa pointi Emmilio Naffat uzito wa bantam.


EmoticonEmoticon