MAKALA YA JAMII
Karibuni katika MAKALA MAALUM kwaajili ya kuelimisha jamii na hasa vijana wa dunia ya leo. Katika makala haya tutazungumzia na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo jamii katika Nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Leo ni siku ya kwanza ya makala yetu katika blog hii na nimatumaini yangu kuwa utanufaika na kujifunza mengi kutoka kwenye makala yetu.
Leo hii ningependelea tuanze safari yetu kwa kuzungumzia maswala ya KIJAMII hususani swala la MAPENZI ambalo kwa kiasi kikubwa swala hili limeteka akili na mawazo ya vijana wengi katika dunia ya sasa.
Uchunguzi na utafiti uliofanywa na wataalamu wetu imeonekana kuwa asilimia kubwa ya vijana wako katika mahusiano ya kimapenzi na wengi wao ni wakati ya miaka 14 hadi miaka 28. Vijana wengi walio katika umri huu utawakuta wana wapenzi zaidi ya mmoja kwa jinsi zote (yaani jinsia ya kike na jinsia ya kiume) ni wachache sana ambao wana mpenzi mmoja na wenye mapenzi ya kweli, hii inatokana na kijana kutojitambua na kujua yeye ni nani na anatakiwa afanye nini.
Watu wanapokuwa katika mahusiano lengo lao na matazamio yao ni kuja kuanzisha familia yao kwa maisha ya baadae. Kabla kijana hajawa na mpenzi ambaye watakuja kuanzisha familia yao ya baadae anatakiwa ajitambue yeye ni nani na huko anakotaka kwenda anatakiwa ajue anaenda kufanya nini.
Kikubwa ambacho nataka tujifunze leo ni kuhusu namna ya kuandaa ndoa au nyumba yenye furaha.
Mambo mengi katika maisha yanatokana na ujana, Kufanikiwa kwa maisha yako inategemea na namna ulivyo utumia ujana wako (USEJA)
Lengo la makala haya ni kukuelimisha na kukufundisha ili uweze kutengeneza ujana wako na maisha yako ya baadae.
SASA TWENDE PAMOJA ILI TUJIFUNZE KATIKA MAKALA HAYA
Je, useja ni nini?
USEJA ni ile hali anayokuwa nayo mtu kabla ya kuoa au kuolewa. Kabla kijana ajaamua kuoa au kuolewa kitaalamu na kifasaha huwa tunamuita MSEJA.
Je, kuna umuhimu wowote wa mtu kuwa mseja?
Jibu la swali hili ni NDIO. Umuhimu upo tena mkubwa kwa mtu anapokuwa mseja kwani:-
- Kwanza ni msingi wa kutengeneza familia
- Ni muhimu kwa ajili ya kuleta maendeleo ya mwanadamu (mtu binafsi), jamii na taifa kwa ujumla
- Ni muda wa kutekeleza au kufanikisha malengo uliyonayo katika maisha
Tusonge mbele kwa kujifunza kitu kingine ambacho ni muhimu kukijua katika maisha wewe kama kijana.
Kabla hujaamua kuoa au kuolewa ni lazima utambue kuwa sisi kama wanadamu tuna mahitaji ya aina tofauti kwa jinsi zote mbili (yaani jinsia ya kike na jinsia ya kiume). Wanaume wana mahitaji yao na kadhalika Wanawake wana mahitaji yao.
Je, wajua tofauti tulizo nazo sisi kama wanadamu? Fuatana nasi ili uweze kujua tofauti tulizo nazo.
TOFAUTI YA KIMAHITAJI
Mwanaume ana mahitaji yake muhimu aliyozaliwa nayo kadhalika mwanamke naye vivyo hivyo.
MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAUME AMEZALIWA NAYO (NATURALLY)
KUHESHIMIWA: - Mwanaume amezaliwa na hulka ya kuheshimiwa na siyo kudharauliwa kwa hiyo wewe kama mwanamke kabla hujaolewa ni lazima ujue kuwa wanaume wanapendwa kuheshimiwa kwani hii itakusaidia kuandaa nyumba bora na familia yenye furaha daima.
ANAMPENDA SANA MTU ANAYEFAHAMU ANACHOPENDA YAANI ANAYEFAHAMU HOBBIES ZAKE: - Wewe kama mwanamke unatakiwa kujua kitu anachopenda mpenzi wako ambaye unatarajia kuwa atakuwa mume wako unatakiwa ujue kuwa huyo mpenzi wako anapendelea nini na mara nyingi unatakiwa uvifanye ili uzidi kumuweka karibu na wewe na hapo mtatengeneza familia bora na yenye furaha.
HAJA YA KUJAMIIANA: - Wanaume wengi wanapokuwa kwenye mahusiano na wanapopata nafasi ya faragha na wapenzi wao mara nyingi wanawaza kufanya nao mapenzi kwa hiyo wewe kama mwanamke unatakiwa ujue namna ya kukaa na mpenzi wako hasa mnapokuwa pamoja faragha kwani si lazima mfanye mapenzi, tafuta namna ya kumfanya mawazo hayo yamtoke na hii itakusaidia wewe kujiepusha aidha na mimba usiyotarajia au pia magonjwa na kukuweka katika namna ya kufanikiwa katika mipango yako ya baadae.
Hayo ni mambo matatu muhimu ambayo mwanaume amezaliwa nayo na wewe kama mwanamke ni lazima uyajue ili uweze kutengeneza familia iliyobora na yakuigwa na jamii kwa kuwa mtakuwa na amani na furaha maisha yenu yote.
Je, wewe kama mwanaume unajua mambo muhimu mwanamke aliyozaliwa nayo? Kama siyo twende pamoja ili uweze kujua mambo hayo;-
MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAMKE AMEZALIWA NAYO (NATURALLY)
KUPENDWA ;- Mwanamke amezaliwa na hali ya kupenda kupendwa, kujaliwa na kuthaminiwa na mwanaume anayempenda, hivyo wewe kama mwanaume ni lazima umpende, umheshimu, umjali na kumthamini mwanamke unayempenda na siyo kumnyanyasa na kumfanya mtumwa kwani kwa kufanya hivyo ni rahisi kujeruhi moyo wake na hamtaishi kwa furaha lakini ukifanya kama nilivyokushauri hapo juu basi maisha yenu yatakuwa ya furaha siku zote.
KUPENDWA KUZUNGUMZISHWA: - Wanawake wengi wanapendwa kuzungumzishwa pindi wanapokuwa na wapenzi wao kwani kwa kufanya hivyo anaondoa mawazo ya kuwa huyu mwanaume hanipendi mbona yuko kimya anapokuwa na mimi au anamuwaza mtu mwingine? Hivyo wewe kama mwanaume ni lazima ujue kuwa unapokuwa na mpenzi wako unatakiwa umzungumzishe tena maneno ya kumtia moyo yahusuyo maisha yenu ya baadae kwani kwa kufanya hivyo utasababisha kubadilisha mtazamo wake na kukuwaza wewe tu na mtaishi maisha ya furaha na amani.
HUBA kwa kiingereza wanasema INFECTION; - Wanawake mara nyingi wanapokuwa na wapenzi wao hupenda wapenzi wao wawafanyie mambo mbalimbali kwa mfano Mwanamke anafurahi sana anapotembea na mpenzi wake hususani mbele za watu amshike mkono na kutembea pamoja au amshike kiuno basi hapo anakuwa anapata raha na furaha na kwa kufanya hivyo wewe kama mwanaume unamtengenezea mazingira ya kukuamini zaidi na kukupenda pia na hii itasaidia na kusababisha kuishi maisha ya furaha siku zote.
Hayo ni mambo matatu muhimu ambayo mwanamke amezaliwa nayo na wewe kama mwanaume ni lazima uyajue ili uweze kutengeneza familia iliyobora na yenye furaha wakati wote na kupendwa na jamii nzima.
Kwa leo naomba tuishie hapo lakini usikose kuungana nasi tena siku ya jumatano ili tuweze kuendelea kujifunza mambo mengi zaidi ya haya ya leo
Hii ni sehemu ya kwanza ya mfululizo wa mambo mengi tunayoenda kujifunza mbeleni
Kama una maswali, ushauri au maoni private tafadhali tuwasiliane kupitia
nrodgers52@yahoo.com
+255 764 288 054
+255 658 288 054
Imetayarishwa na kuandaliwa na:
Rodgers Israel Nelson
EmoticonEmoticon