MTU MMOJA AFARIKI DUNIA HUKO MIRERANI

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Musa mwenye umri kati ya miaka(26-27)amefariki dunia katika machimbo ya madini ya Tanzanite, huko Mirerani mkoani Manyara baada kukosa hewa .

      Mtu huyo alifariki dunia wakati alipokua akipanda juu kutoka chini ya mgodi huo wa Tanzanite  akiwa  na wachimbaji wenzake ,na kabla ya kufikwa na mauti hayo aliwaambiwa wenzake kuwa anajisikia vibaya  na aliomba kupumzika na ndipo mauti yalipomkuta .

     Tayari polisi wameshafika katika eneo la tukio hilo ambalo mmliki wa mgodi huo  ametambulika kwa jina la bwana ISAAC ,huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo .


    Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru na tayari polisi wamefunga mgodi huo kwa uchunguzi zaidi.


    Tukio hilo limetokea zikiwa ni siku chache tu tangu kutokea kwa kifo cha mtu mmoja na kuacha wengine sita wakiwa majeruhi.



EmoticonEmoticon