Wananchi katika kata ya Shangarai eneo la Ngwandua , wamevamia shamba la muwekezaji mmoja kwa madai kuwa muwekezaji huyo amekiuka masharti ya kupewa shamba hilo.
Wakiongea na Blog hii wananchi hao katika eneo la tukio wamesema kuwa walimpa muwekazaji huyo eneo hilo kwa madhumini ya kulima kahawa ,lakini muwekazaji huyo amekiuka masharti na kupanda miti badala ya kupanda kahawa kama makubaliano yalivyokuwa.
Wananchi hao wameyavamia mashamba hayo wakiwa na silaha za jadi kama mapanga ,rungu,majembe ,shoka ,mishale na mikuki .
Tukio hilo limenza jana usiku saa tano wananchi hao walipovamia eneo hilo na kutaka kumtoa mmliki wa shamba hilo kwa maelezo kuwa hawamuelewi kwanini apande miti badala ya kupanda kahawa kama makubaliano yalivyokuwa yamewekwa na serikali.
Muwekezaji huyo aliyefahamika kwa jina la HANSI DETIE ,ametoweka katika eneo hilo la tukio alipokuwa anaishi kwa kuhofia usalama wa maisha yake na hadi hivi sasa haijulikani amekimbilia wapi kwa kuhofia wananchi hao wenye hasira kali.
Jeshi la polisi mkoani Arusha ilibidi watumie nguvu za ziada kuweza kutuliza ghasia hizo ambazo zilianza kuanzia saa tano usiku na hadi kufikia leo majira ya saa tano wakafanikiwa kutuliza ghasia hizo za wananchi hao wenye hasira kali.
EmoticonEmoticon