Pep Guadiola kocha wa Fc Barca
Kocha wa klabu ya Fc Barca Pep Guadiola amekanusha tetesi zinazovuma yakwamba anaelekea kunako klabu ya darajani The Blues baada ya kutangaza anaikacha klabu ya Barca mwishoni mwa msimu huu.
Pep Guadiola anaondoka Fc Barca baada ya kuitumikia kwa miaka minne (4) akisaidiwa na msaidizi wake Tito Vilanova ambaye atakuwa kocha wa klabu hiyo.
Guadiola ameendelea kusema ana mpango wa kupumzika kwa muda wa mwaka mmoja kwa kudai kuwa uwezo wake kwa sasa umefikia mwisho hivyo anajipanga upya ili awe na makali mengine na mbinu mpya za ufundishaji.
Roman Abromovich-mmiliki wa The blues
Kwa upande wake tajiri la Kirusi Roman Abromovich amesema yupo tayari kutoa kitita chochote cha mkwanja ili akinoe kikosi cha The Blues na kukazia kwamba Guadiola aseme anahitaji kiasi gani ili akifundishe kikosi hicho kilichotinga hatua ya fainali ya klabu bingwa baada ya kuwatoa mabingwa watetezi Fc Barca.
Guadiola anatarajiwa kurithi mikoba ya kocha aliyetimuliwa AVB na nafasi yake kushikiliwa na kocha msaidizi Di Mateo ambaye anafanya vizuri na kikosi hicho na kufanikiwa kukifikisha hatua ya fainali ya mabingwa.
Guadiola amepata mafanikio makubwa kwa kipindi alichokaa na Barca baada ya kuipatia timu hiyo jumla ya mataji 13 kwa misimu minne (4).
EmoticonEmoticon