Naibu mkurugenzi wa Takukuru Bregedia John Mbungo |
Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa nchini (TAKUKURU) imetengaza zawadi nono ya shilingi milioni kumi kwa mtu atayewezesha kupatikana kwa aliyekuwa mhasibu wa taasisi hiyo, Godffrey Gugai anayedai kuwa na ukwasi mkubwa wa fedha na mali isiyolingana na kipato chake halali akiwa kama mtumishi wa umma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bregedia John Mbungo amesema, baada ya kuchunguza na kutoa taarifa ya awali walimuita Gugai na kumuhoji ambapo alionyesha ushirikiano wa kujibu hoja hizo zinazomkabili na kuwa na mali nyingi kuliko kipato chake.
Amesema, kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha sheria ya Kuzuia na kupaambana na Rushwa ni kosa la jinai kwa afisa wa serikali au mtumishi wa umma kuwa na mali nyingi au maisha ambayo yanazidi kipato chake bila ya kuwa na maelezo yoyote anayoelezea mali zile amezipata wapi au kwa namna gani.
“Bwana Gugai aliweza kujikusanyia mali nyingi ambazo awali tulijaribu kumuuliza na alielekea kuonyesha ushirikiano lakini baadae alipoona kwamba hana maelezo ya namna gani amezipata zile mali akapotea. tumeendelea kumtafuta na taarifa ambazo tumekuwa tukizipata amekuwa ni mtoro amekimbilia nje ya nchi kupitia njia ambazo siyo rasmi” amesema Bregedia Jenerali Mbungo.
Mhasibu huyo anamiliki maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki pamoja na viwanja 37.
Amesema ni kosa kubwa kwa mtumishi wa umma kutumia ofisi yake kujipatia mali nje ya kipato akipatacho ni kosa, aliwahi kuchukuliwa maelezo, alipogundua hana maelezo sahihi akaamua kukimbia.
Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi, Kiseke jijini Mwanza, Arusha na Tanga.
Hata hivyo, mali za Gugai zimewekewa zuio la mahakama na mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.
Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.
EmoticonEmoticon