Wananchi wa kata ya Bolisa wanatarajia kujengewa shule mpya ya sekondari ya kata ili kuondokana na tatizo la umbali kwa wanafunzi wa kata hiyo, amebainisha na Mkurugenzi wa Mji Kondoa Bw. Khalifa Kondo alipokuwa akijibu swali wakati wa mkutano wa wananchi wa kata ya Bolisa na Mkuu wa Mkoa alipofanya ziara ya kujitambulisha wilayani humo hivi karibuni.
"Shule ya Gubali imeshughulikiwa na wananchi wa kata ya Gulisa kabla ya kugawanywa kuwa kata mbili lakini kwasasa kata ipo kata ya Kolo tunaomba kujua mipaka ya kata hizi mbili ili shule ya Gubali ibaki Bolisa".aliuliza bwana Abubakari Mussa.
Akifafanua Bwana Kondo alisema kuwa ni kweli shule hiyo ipo lakini kutokana na mazingira ya shule hiyo wameanza kupata fedha za kujenga mabweni katika shule ya Sekondari Gubali kwa ajili ya wanafunzi kutoka nchi nzima na si Kolo tu.
Kondo aliendelea kufafanua kuwa kutokana na mipango hiyo wilaya imejipanga kujenga shule mpya ya Sekondari kwa ajili ya wananchi wa kata ya Bolisa kwa ajili ya kuwasogezea huduma wananchi kwa ukaribu kwani ndio lengo la serikali ya awamu ya tano.
Aidha aliongeza kuwa Rais amemwagiza Waziri wa ujenzi kuiachia wilaya majengo yaliyokuwa yanatumiwa na kampuni ya ujenzi wa barabara eneo la Kolo ili yatumike kwa ajili ya kuanzisha shule ya sekondari kwa wanafunzi wenye vipaji maalum toka nchi nzima.
Baada ya ufafanuzi huo Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge alipongeza mpango huo na kuwataka kuutekeleza kwa ushirikiano ili wananchi wapate huduma inayostahili.
Shule ya Sekondari Gubali ni shule ya Sekondari iliyopo katika kata ya Kolo ikihudumia wananchi wa kata hiyo na kata ya Bolisa ambapo imejengwa juu ya mlima hali inayowapa shida wanafunzi kufika shule.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Nobility Mahenge kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota wakati wa ziara yake wilayani humo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mwalimu Kibasa akijibu swali kwenye mkutano wa wananchi na mkuu wa Mkoa katika kata ya Bolisa. |
Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo akifafanua jambo kwenye mkutano wa wananchi na Mkuu wa mkoa |
EmoticonEmoticon