JERRY SANTO ASAJILIWA COASTAL UNION


Klabu ya Coastal Union jana imetangaza rasmi usajili wa kiungo wa kimataifa wa Kenya Jerry Santo, ambaye msimu wa 2010-2011 alikuwa mmoja ya viungo bora wa klabu bingwa ya soka ya Tanzania klabu ya Simba.

Santo ambaye aliondoka Simba kwa madhumuni ya kwenda kucheza soka nchini Albania kabla ya mambo kumuendea sivyo na kurudi Tusker ya Kenya. Amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.

Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa facebook wa klabu ya Coastal mchezaji huyo anakuwa wa mwisho katika usajili wa mwaka huu.


EmoticonEmoticon